Jumanne 26 Agosti 2025 - 00:25
Ofisi ya Ammar Hakim: Uongo Kuhusu Msimamo wa Tofauti wa Ammar Hakim Kuhusu Vikosi vya Hashd al-Shaabi Haukubaliki Kwa Njia Yoyote

Hawza/ Ofisi ya vyombo vya habari ya Rais wa Muungano wa Vikosi vya Kitaifa vya Iraq imekataa uvumi unaosema kwamba Sayyid Ammar Hakim, kiongozi wa muungano huo, ana msimamo tofauti kuhusu vikosi vya Hashd al-Shaab

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, ofisi ya vyombo vya habari ya Sayyid Hakim imethibitisha kuwa uvumi unaosema kwamba Sayyid Ammar Hakim ana msimamo tofauti kuhusu vikosi vya Hashd al-Shaabi haupo sahihi.

Katika tamko lililotolewa na ofisi ya vyombo vya habari ya Sayyid Hakim, limeeleza kuwa: “Kulingana na mtazamo wa Hujjatul Islam Sayyid Ammar Hakim kuhusu vikosi vya Hashd al-Shaabi, ambavyo anavyiona kuwa ni hitaji la kiusalama na kimkakati kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa la Iraq, na kwa kutambua sadaka kubwa zilizotolewa na mashujaa, viongozi, na wanachama wake katika kuliongoza taifa kutoka mikononi mwa ugaidi, tunasisitiza uthibiti wa msimamo huu thabiti.”

Tamko hilo liliendelea kusema: “Tunakumbusha pia nafasi ya Sayyid Hakim katika kupitisha sheria ya Hashd al-Shaabi mwaka 2016 na ulinzi wake endelevu wa taasisi hii ya kitaifa kama mojawapo ya nguzo za mfumo wa ulinzi wa Iraq, kwa hivyo, tunakataa uvumi wowote unaosema kuhusu misimamo tofauti ya Sayyid Hakim kuhusu vikosi vya Hashd al-Shaabi, nafasi muhimu ya vikosi hivi, na kuhifadhi haki za wanachama wake, tunasisitiza kuwa uvumi huu wote hauko sahihi kabisa.”

Tamko hilo liliendelea: “Pia tunaviomba vyombo vyote vya habari kuhakikisha usahihi katika kuchapisha habari na kuthibitisha kuwa taarifa zinatolewa kutoka vyanzo rasmi na vinavyotegemewa.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha